Vyama vikuu vya Upinzani nchini Tanzania vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD ambavyo vinaunda UKAWA vimeidhinisha rasmi makubaliano ya ushirikiano katika maneneo saba ikiwa ni mkakati wa kuelekea chaguzi mbalimbali zijazo.
wakizungumza katika nyakati tofauti wakati wa mkutano wao mkubwa uliofanyika katika viwanja vya Jangwani jijini Dar-es-Salaam, viongozi wakuu wa vyama hivyo walitia saini makubaliano ya ushirikiano wa kuunganisha sera zinazofanana za vyama hivyo ili kuwa na kauli moja kitaifa, kusimamisha wagombea wa pamoja katika ngazi zote za uchaguzi kulingana na kukubalika kwa chama katika eneo/jimbo husika, kuunganisha nguvu na kuwaelimisha wananchi kuikataa Katiba pendekezwa, kujenga ushirikiano wa vyama hivyo katika masuala ya kitaifa kwa maslahi ya watanzania wote, pamoja na kuulinda muungano usiokuwa na migogoro kama ilivyo sasa. Habari zaidi ingia humu..
Katika hatua nyingine katibu mwenezi wa CCM Nape Nnauye amesema kwamba hatua ya vyama hivyo kuungana ni dalili za kuelekea kupoteza mwelekeo kwani hata mwitikio mdogo wa watu kwenye mkutano huo unadhihirisha hilo.
Picha kwa hisani ya Mwananchi newspaper online